Sunday, December 22, 2013

TUSHIKAMANE SEKONDARI IMESHINDA SHINDANO LA INSHA AFRIKA MASHARIKI, IMEZIBWAGA SHULE NNE ZA SEKONDARI KUTOKA KENYA, RWANDA, BURUNDI NA UGANDA.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi Peter Robert wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari ya kata Tushikamane ya mjini Morogoro baada kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la Insha kuhusu Ujenzi wa Miundombinu Afrika Mashariki.Mwanafunzi Peter amechukua ushindi wa kwanza kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wa nchi tano za jumuiya ya Afrika Mashariki .

Peter alipokea tuzo hiyo wakati wa Mkutano wa wa kuu wan chi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Speke’s Bay Resort,Munyonyo, Kampala Uganda juzi.Kutokana na ushindi huo Mwanafunzi huyo amepewa tuzo ya dola za Marekani 1500, na cheti na alikabidhiwa zawadi hizo na mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.




No comments:

Post a Comment