Tuesday, October 23, 2012

ESTER EMMANUEL AMESHINDA SHINDANO LA INSHA AFRIKA MASHARIKI (2012)



Mwanafunzi Ester Emmanuel wa kidato cha nne wa shule ya sekondari ya Tushikamane ya Mkoani Morogoro ameshinda nafasi ya pili kitaifa katika shindano la uandishi wa INSHA. Shindano lili wataka kuandika INSHA yenye maneno 1500-2000 kuhusu NAFASI YA ELIMU ATIKA KUIMARISHA MTANGAMANO WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI. Shule itapewa vifaa vyenye thamani ya US$ 1000 na mwanafunzi US$250 kama zawadi, pia mwanafunzi Ester Emmanuel na washindi wengine wanne watadhaminiwa ziara ya kutembelea nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Insha tano bora kutoka Tanzania zimepelekwa ARUSHA kushindana na nyingine tano bora kutoka kila nchi mwanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Iwapo Ester Emmanuel atashinda tena katika hatua hii katika nafasi ya kwanza atapata zawadi ya US$1200 nakupata fursa ya kukutana na Maraisi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. HONGERA SANA SHULE YA SEKONDARI YA TUSHIKAMANE.




ESTER  EMMANUEL

No comments:

Post a Comment