Monday, June 4, 2012

MKUU WA SHULE TUSHIKAMANE SEKONDARI AMELEZA KUWA KUFAULU KWA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WAKATI HAWAJUI KUSOMA NAKUANDIKA NI MATOKEO YA MFUMO MBAYA WA ELIMU

Mkuu wa shule ya Tushikamane Sekondari Bw. Joseph Simoni Moga, amewaeleza walimu wa shule ya yake kuwa kufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba wakati hawajui kusoma na kuandika ni matokeo ya mfumo mbaya wa elimu, Bw. Moga ameeleza kuwa mtihani wa darasa la nne unao wachuja wanafunzi kuendelea na madarasa ya juu sasa hauna mchujo wowote kwani wanafunzi wote (walio feli na walio faulu) wanaendelea na masomo ya madarasa ya juu bila kuwapa fursa ya kukalili darasa kwa wale walio feli, hivyo basi wanafunzi wasio jua kusoma na kuandika huendelaea kusonga mbele hadi kufika darasa la saba wangali hawajui kusoma na kuandika, pia Bw. Moga Ametupia lawama Baraza la mitihani NECTA kwa kutunga mitihani inayo wataka watahiniwa wa darasa la saba kuchagua jibu sahihi kwa kuandika HERUFI ya jibu hilo katika kijitabu cha kujibia maswali mbele ya namba ya swali husika. "Hii pia inachangia kwa kiasi kubwa kwa wanafunzi wengi wa darasa la saba kufaulu wakati hawajui kusoma na kuandika, kwani ni rahisi kuigilizia toka kwa mwanafunzi mwenye uwezo na kubashiri jibu sahihi" Alisema Bw. Moga.

No comments:

Post a Comment