Sunday, May 13, 2012

TANGAZO KUHUSU USAJILI NECTA 2012 KWA WATAHINIWA WOTE WA KUJITEGEMEA

Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia Watahiniwa wote wa Kujitegemea wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi Februari, 2013 kwamba kipindi cha usajili kilianza rasmi tangu tarehe 01/04/2012, kipindi cha malipo bila adhabu kinaishia tarehe 31 Mei, 2012. Kuanzia tarehe 01 Juni, 2012 hadi tarehe 30 Juni, 2012 waombaji watajisajili kwa ada ya shilingi 50,000/= (ada pamoja na faini).

 Usajili unaendelea kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya: www.necta.go.tz

 Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) watakazotumia kujisajili. Hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kupata namba rejea kutoka katika kituo anachokusudia kufanyia mtihani. Wakuu wote wa vituo vya watahiniwa wa kujitegemea nchini wamekabidhiwa namba rejea hizo tayari kwa kuzigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo.

 LIMETOLEWA NA:

 KATIBU MTENDAJI
 BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA









No comments:

Post a Comment